Home » » MKUTANO WA KINANA KATORO, GEITA WAVUNJA REKODI YA WATU‏

MKUTANO WA KINANA KATORO, GEITA WAVUNJA REKODI YA WATU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita.

Komredi Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wilayani Geita, ambapo aliwadhihaki wapinzania kwamba watashindwa vibaya katika uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu akidfai hawana sera wala mipango inayoeleweka ya kuwasaidia watanzania kupiga hatua za kimaendeleo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika katika mkutano wa hdhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.

 Wananchi  wa Kijiji cha Shinyamwendwa, Kata ya Nyanguku wakitoa malalamiko yao baada ya kuzuia msafara wa Komredi Kinana,  kuhusu  ubovu wa barabara, kutopatikana kwa mawasiliano katika Kijiji hicho, katika Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.
 Komredi Kinana akilakiwa na wananchi wa Kijiji cha Nyankanga ambapo alishiriki  kulima barabara ya Kijiji wilayani Geita, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Busanda.

 Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Geita, Vick Kamata akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Nyankanga, Jimbo la Busanda mkoasni Geita leo.
 Mwandishi wa Habari wa Clouds TV, Salum Mwinyimkuu, akiwaonesha wasanii picha mbalimbali alizowapiga walipokuwa wakitumbuiza wakati msafara wa Komredi Kinana  ulipowasili katika Kijiji cha Nyankanaga, Jimbo la Busanda, Mkoa wa Geita. Kutoka Kulia ni Manaeno Richard 'Ngembele' na Sadick Malehiwa.
 Komredi Kinana (wa tatu kulia), akishiriki kulima barabara ya Kijiji cha Nyankanga, wilayani Geita wakati wa ziara yake katika Jimbo la Busanda.
 Sehemu ya eneo la machimbo ya Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico ambalo lina mgogoro na wachimbaji wadogo wadogo ambalo Komredi Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi.
 Komredi Kinana akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo wa madini kuhusu mgogoro wao na Shirika la Madini la Stamico kuhusu mgogoro huo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipiga picha ya video wakati Komredi Kinana akizungumzia mgogoro wa machimbo ya madini ya Nyaruguru, wakati wa ziara katika Jimbo la Busanda, wilayani Geita.
 Baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini, wakisikiliza wakati Komredi Kinana akzungumza nao kuhusu mgogoro wao na Stamico.

 Komredi Kinana akihutubia wananchi alipofika katika Kijiji cha Chikobe , Kata ya Chiluma katika Jimbo la Busanda.
 Komredi Kinana akishiriki kupiga lipu  Jengo la Watumishi wa Idara ya Afya katika Kijiji cha Inyala, Jimbo la Busanda Wilayani Geita leo/
 Wananchi akizungumza na akina mama wajasiriamali katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda, Geita leo, ambapo amewaahidi kuwakutanisha na Mfuko wa Taifa wa  Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili wapatiwe mkopo wenye riba nafuu.
Nape akiongozana na Komredi Kinana na wananchi wengine kwenda kwenye mkutano mjini Katoro, Geita
 Komredi Kinana akitembea kwa miguu kwenda kwenye mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro.
 Komredi Kinana akiwasalimia wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Katoro.
 Mbunge wa Jimbo la Busanda, Lowrencia Bukwimba akielezea miradi mbalimbali aliyotekeleza katika kipindi chanke cha ubunge.
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya nyumba walipokuwa wakisikiliza hotuba ya Komredi Kinana katika Mji wa Katoro

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa