WATU wanaosadikika kuwa wa
kikundi cha Chinja Chinja wamefanya mauaji ya kutisha baada kumuua mwanamke,Mondesta
Nchambi (53) mkazi wa kitongoji cha Isabilo kijiji cha Nyakarango wilayani
Chato mkoani Geita,kwa kumchinja shingo kwa kutumia kitu chenye ncha kali kisha
kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake.
Mauaji hayo ya kusikitisha
yametokea usiku wa kuamkia leo(Alhamisi)ambapo mwili wa marehemu huyo ulikutwa
ukiwa umetelekezwa kandokando ya kichaka kilichopo umbali wa mita 300 kutoka
nyumbani kwake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita,
Leonard Paulo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa watu
wasiofahamika walifanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Kamanda Paulo amesema taarifa za awali zimeonyesha kuwa
kabla ya kukutwa na mauti hayo mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juzi
majira ya mchana.
Kabla ya kukutwa na mauti mwanamke huyo alielekea kwenye gulio la wakulima lililopo kweye kijiji jirani cha Kazunguti,lakini wakati wa kurejea nyumbani kwake usiku alikutana na watu hao ambao walimchinja shingoni na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Inasadikiwa kuwa wauaji hao
waliondoka na kichwa cha mwanamke huyo kutokana na polisi wilayani Chato kwa
kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho kukitafuta kwa zaidi ya saa 6 pasipo
mafanikio ya kukipata.
Kikundi cha Chinja Chinja kinadaiwa kujihusisha na mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Kanda ya ziwa kama Simiyu,Geita,Shinyanga,Mara na Mwanza kwa kukodiwa na watu kutokana na imani za kishirikina.
Kikundi cha Chinja Chinja kinadaiwa kujihusisha na mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Kanda ya ziwa kama Simiyu,Geita,Shinyanga,Mara na Mwanza kwa kukodiwa na watu kutokana na imani za kishirikina.
0 comments:
Post a Comment