Home » » TNBC MBIONI KUZINDUA BARAZA LA BIASHARA SIMIYU

TNBC MBIONI KUZINDUA BARAZA LA BIASHARA SIMIYU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC), linatarajiwa kuzindua baraza la biashara la Mkoa wa Simiyu hivi karibuni na kufanya mikoa yote kuwa na mabaraza hayo.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Raymond Mbilinyi, aliwaambia waandishi wa habari mkoani Geita hivi karibuni kuwa, taratibu za kuzinduliwa kwa baraza katika Mkoa wa Simiyu zimefikia pazuri.
“Tumebaki na Mkoa mmoja wa Simiyu katika kuhakikisha mabaraza yote nchini yanafanya kazi,” alisema wakati wa uzinduzi wa baraza la biashara la Mkoa wa Geita.
Alifafanua kuwa, serikali imejiwekea mkakati wa kuhakikisha mwaka 2025, nchi inafikia uchumi wa kati ambao pia utawaletea maisha bora zaidi watanzania.
Alisistiza kuwa, mabaraza ya biashara ya mikoa yanawajibu wa kuwa kichocheo cha sekta binafsi kuimarika zaidi na inachangia ukuaji wa uchumi. Mabaraza ya biashara ya Mkoa yanaundwa na wadau kutoka sekta ya umma na binafsi na yanafanya kazi kwa kusimamiwa na TNBC.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Severine Kahitwa, alihamasisha wawekezaji kwenda katika mikoa mipya iliyoanzishwa. Geita na Simiyu ni kati ya mikoa mipya kuanzishwa na Serikali Tanzania bara.
Mmoja wa wajasiriamali wa Geita, Chacha Wambura, alisema nchi ikiwa na watu wake wengi waliowekeza, itasaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa watu wengi.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa