Home » » JUKATA YAPELEKA WARAKA KUTAKA BUNGE LA KATIBA LIAHIRISHWE

JUKATA YAPELEKA WARAKA KUTAKA BUNGE LA KATIBA LIAHIRISHWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba,
 
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limeendelea kuushinikiza uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kutumia mamlaka yake kisheria kuahirisha Bunge hilo kabla ya mwisho wa mwezi huu hadi baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba, ilieleza kuwa Jukwaa hilo limeandika waraka kwenda kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kipindi cha kuahirishwa kwa Bunge hilo, serikali zote mbili ziendeshe zoezi la kupiga kura ya maoni ili wananchi wa pande zote mbili waamue juu ya aina ya Muungano wanaoutaka.

Alisema uchaguzi wa serikali za mitaa uliopaswa kufanyika Oktoba, mwaka huu, na ambao maandalizi yake hayajaanza kikamilifu uahirishwe na kufanyika pamoja na siku moja na uchaguzi wa mwaka 2015.

Alipendekeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutunga sheria itakayoweka ratiba mpya na ulazima kwa uongozi utakaochaguliwa mwaka 2015 kuendeleza mchakato wa katiba mara baada uchaguzi mkuu.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa