Home » » DIWANI, MTENDAJI WARUDISHA FEDHA WALIZOIBA GEITA

DIWANI, MTENDAJI WARUDISHA FEDHA WALIZOIBA GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SIKU chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari iliyokuwa ikiwatuhumu Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maweda Gwesandili na Mtendaji wa Kata ya Isulwabutundwe, Sadik Masalu kuiba sh. milioni 1.2 za wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wameanza kuzirudisha.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili, umebaini kuwa viongozi hao hadi sasa wamesharudisha sh. 800,000.
Kaimu Mtendaji wa kata hiyo kwa sasa, Joel Nguku, alisema kuwa Diwani Maweda na mtendaji wake wameamua kurudisha pesa hizo baada ya Tanzania Daima kuandika wizi huo na wananchi kutishia kuwaburuza mahakamani kutokana na wanafunzi hao kukosa masomo.
Nguku, aliongeza kuwa pamoja na viongozi hao kuanza kurudisha pesa hizo, lakini Masalu ambaye ni mtendaji amekataliwa na wananchi wa kata hiyo kuendelea kukaa hapo.
Nguka amelipongeza gazeti la Tanzania Daima kwa kutoa taarifa hiyo iliyosaidia watuhumiwa hao kuanza kurejeshwa kwa fedha za wanafunzi hao.
Tanzania Daima Jumapili, lilimuuliza Diwani Maweda kuhusu kurudisha pesa hizo ambapo alikiri kurudisha shilingi laki nne ambazo alisema alikuwa amezikopa na nyingine zinazobaki anatakiwa arudishe mtendaji wake ambaye alichukua nyingi zaidi.
Naye mtendaji alipoulizwa lini atarudisha pesa alizokwapua alisema kuwa pamoja na kuzichukua pamoja na diwani, lakini anashangaa kuona mpira unaangukia kwake.
“Mimi namshangaa diwani wangu anasema kuwa mimi nilichukua pesa nyingi na huku tuligawana, wote tunatakiwa turudishe nusu kwa nusu, sijui kwanini diwani anawaambia wananchi kwamba pesa zote niliiba mimi, huo ni uongo,” alisema Masalu.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa