Home » » UTUMIKISHAJI WATOTO WASHAMIRI GEITA

UTUMIKISHAJI WATOTO WASHAMIRI GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WILAYA ya Geita imebainika kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo utumikishwaji wa watoto wadogo kwenye maeneo ya migodini unazidi kushamiri.
Hayo yamebainika katika utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la Nelico lililopo mjini Geita kwa kushirikiana na Shirika la Codert na Plan International kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Utafiti huo uliofanywa mwaka 2009, umebaini kuwa wanafunzi walioacha shule na wale watoro sugu katika kata 11 za wilaya za Geita na Nyangh’wale huku kukiwa na vijiji 51 na shule 65.
Ofisa Mradi katika mradi wa kuzuia ajira hatarishi kwa watoto hususan migodini, Mbuya Viane, alisema baada ya kufanya utafiti huo wamegundua ndani ya kata hizo 11 wanafunzi 12,300 wamepotelea katika shughuli za migodini na uvuvi.
Mbuya alisema hadi sasa ni wanafunzi 5,191 tu ambao wamefanikiwa kurudi shuleni tangu mwaka 2012 na 2013 huku akibainisha kuwa kati yao 2,231 walikuwa wameacha shule kabisa.
Alieleza kuwa watoro sugu ni 2,960, ambao ni wanafunzi kuanzia darasa la tatu hadi la saba.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa